Shirika la Transaid lina furaha kukualika katika kongamano litakalo fanyika kupitia mtandao. Mada yake ikiwa Texi za Pikipiki katika Muktadha wa vijiji vya Asia kusini na mataifa ya kiafrika kusini mwa sahara
Shirika la Transaid lina furaha kukualika katika kongamano litakalo fanyika kupitia mtandao. Mada yake ikiwa Texi za Pikipiki katika Muktadha wa vijiji vya Asia kusini na mataifa ya kiafrika kusini mwa sahara. Hili litakuwa Utafiti la Kufikia Jumuia kupitia Ushirikiano (ReCAP). Lilifadhiliwa na idara ya maendeleo ya kimataifa la Transaid.
Kongamano hili la saa tatu kamili mtandao litafanyika alhamisi Aprili tarehe sita, saa sita adhuuri. Na litawakusanyisha wataalam wa utafiti wa usafiri wa kiafrica na kiasia, kutoka vyuo vya utafiti na vyuo vikuu.
Watakao kuwepo kwenye Jopo letu la wataalamu ni; Bw. Leo Ngewi kutoka shirika la kudhibiti usafiri barabarani na majini (SUMATRA) la Tanzania, Daktari Elizabeth Ekirapa Kiracho kutoka chuo kikuu cha Makerere Uganda na Bw. Felix Wilhelm Siebert kutoka chuo kikuu cha ufundi cha Berlin Ujerumani. Majadiliano yataongozwa na Caroline Barber, Mkuu wa Mipango Transaid atakaye wakaribisha wahusika kuuliza maswali na pia kuchangia mawazo yakuboresha utafiti wa mada hii.
Katika Mataifa mengi pikipiki na teksi- pikipiki (zinazojulikana kama bodaboda) ndio vyombo vya usafiri vinavyotumika sana. Asilimia sabini na tano ya wasafiri vijijini hutumia vyombo hivi. Huu ndio wakati mwafaka wa kujadili jinsi Bodaboda inaweza kutumika kubadili maisha ya umaa na pia kujaribu kuzuia ajali na kuboresha usalama.
Tumeskia ana kwa ana jinsi mataifa mengine yameweza kuangazia na kudhibiti ongezeko la bodaboda na ni mafunzo yepi waliyojifunza. Utumizi wa teksi-pikipiki katika Asia kusini na mataifa ya kiafrika kusini mwa sahara, umeongezeka haraka kwa miaka iliyopita. Sehemu ambapo usafiri ulikuwa mgumu, hapo awali, hivi sasa, bodaboda zinatoa huduma za usafiri kwa urahisi, haraka na wa nyumba kwa nyumba.
Utumizi wa bodaboda kwa njia hii ni maendeleo bora kwa jamii nyingi za Asia kusini na mataifa ya kiafrika kusini mwa sahara. Ingawaje, ongezeko la bodaboda na wepesi wa kusafiri hakukosi maswala ya usalama. Pikipiki ianatambulika kama tishio la usalama kwake dereva na abiria.
Ijawapo kunaongezeko la pikipiki maswali nyeti ya usalma na udhibiti yameulizwa.
Jopo letu la wataalamu makinifu lita angazia maswala ya mafunzo, udhabiti na utumizi wa kofia ya dereva wa bodaboda. Tutaskia kuhusu mabadiliko yatakayoletwa kupitia usafiri wa bodaboda kwa kuwasaidia watu vijijini kufikia huduma za afya.
Pia tutajifunza kuhusu ubunifu na vile teknolojia katika simu za rununu zinabadilisha utumizi wa bodaboda.
Kwa kujisajili tadadhali ubonyeze kiunganishi hii